Ismail Makame Juma mwenye umri wa miaka mitatu amefariki dunia  papo hapo baada ya kutumbukia kwenye shimo la karo lilojaa maji nyuma ya nyumba Huko Chaani Ketwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Akitoa maelezo juu ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Abdallah Haji amesema kuwa tukio hilo limetokea 12-05-2019 majira ya saa nne asubuhi huko chaani Ketwa. “ametumbukia mtoto wa kiume mwenye umri miaka mitatu katika shimo la karo lilopo nyuma ya nyumba”amesema Kamanda huyo.


Sambamba na hayo Kamanda haji amewataka wazee kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha mvua ilikuepusha vifo visivyo vya lazima na kuwataka kuweka uzio katika mashimo yao ya karo za maji .


Na: Rauhiya Mussa Shaaban