DUDUZANE ZUMA (35) mtoto wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana (Jumatatu) alikana kuhusika kutoa ruishwa ya Dola mil. 40 kwa aliyekuwa naibu waziri wa fedha, Mcebisi Jonas .

Duduzane alikuwa akitoa ushahidi mbele ya kamati ya kimahakama inayochunguza madai kwamba baba yake alijihusisha katika ufisadi na kupora fedha za serikali.

Inasemekana kwamba Duduzane aliitoa fedha hiyo kupitia kampuni la Gupta lililo na uhusiano na baba yake ambapo Jonas alipewa fedha hizo katika mkutano uliopangwa na Duduzane.

Inadaiwa nia ya hongo hiyo ilikuwa ni kwa waziri huyo kutoa upendeleo wa kibiashara kwa kampuni hilo ambapo malipo yake yangekuwa kupandishwa cheo na kuwa waziri kamili wa fedha lakini waziri huyo aliikataa fedha hiyo.