Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amesema kuwa mtu yeyote akithibitika kuwa na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) apelekwe eneo maalum bila kujali cheo chake na atalala palipoandaliwa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana(Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.

Aidha Waziri Majaliwa amewataka Watanzania wazingatie masharti ya afya kwa kufuata ushauri unaotolewa na Serikali kwa sababu hivi sasa nchi yetu na dunia kwa ujumla inapitia katika kipindi kigumu pia,waendelee kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii.