Muhogo wazusha mjadala Baraza la wawakilishi

Wizara ya kilimo mali asili ,Mifugo na Uvuvi  imesema hakuna kampuni yoyote ya kichina iliyojitokeza kuwakopesha Fedha wakulima wa zao la Muhogo ili kuimarisha zao hilo Nchini.

Akijibu swali  la Mwakilishi wa Jimbo la Konde Omar Seif Abeid katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa zanzibar ametaka kufahamu kuwa serikali ina Mpango gani  kwa wakulima wa zao la Muhugo kuweza kutumika kwa biashara.

Nae Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dk Makame Ali Ussi amesema serikali haijapokea muekezaji yoyote wala kampuni iliyojitokeza kununua zao hilo kutokana na kampuni hiyo bado haijaanza utaratibu wa kununua muhogo hapa zanzibar.

Amesema ni vyema kwa kampuni binafasi kutumia fursa hiyo kwa kuuunga mkono juhudi za serikali kuwekeza  katika sekta ya Kilimo ili kuwawezesha wakulima kulima zao la chakula na Biashara Nchini.

Aidha amesema Wizara pia itaendelea na Jitihada za kuwatafutia Wakulima mbegu bora itakayowawezesha kulima zao hilo kwa kukidhi  mahitaji ya watumiaji pamoja na kuwapelekea wataalamu wa kilimo wakaowapa mafunzo wakulima.