Mume na mke waliokuwa wakisafiri kwenda kula sikukuu ya krismas wafariki katika ajali. Wanandoa hao waliofariki alfajiri ya leo walikuwa safarini kuelekea Busia kwa ajili ya sherehe za mwisho wa mwaka (Krismasi na Mwaka Mpya)

Watu watano waliokuwemo wote wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea katika Daraja la Mwiwondwe lililopo barabara ya Ekero kuelekea Buyangu nchini Kenya

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Maria wa Mumias. Idara ya Polisi imetoa tahadhari kwa watu wanatumia Vyombo vya Moto kuendesha magari kwa uangalifu