Bingwa wa zamani wa michuano ya kuogelea alijitosa majini baada ya marafiki wa mwanaume huyo kuanza kupiga kelele katika ufukwe wa Cala Sinzias.

Magnini aliunyanyua uso wa Benedetto juu ya maji mpaka wahudumu waokoaji walipowasili.

”Nilianya nilichotakiwa kufanya,” mwanamichezo huyo mstaafu alisema.

Ni siku mbili pekee kabla, bwana Benedetto, 45, alikua amefunga ndoa na mpenzi wake wa jinsia moja.

Tukio hilo la Jumapili lilishuhudiwa na rafiki wa wapenzi hao na mwandishi wa habari wa eneo la uajemi, Soroush Paksad.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Wapenzi hao walikuwa wakielea wakiwa juu ya boya, kabla ya Benedetto kuangukia kwenye maji, yaliyokuwa yabaridi kuliko ilivyotarajiwa, hivyo hakuweza kusogeza miguu yake kutokana na hali ya kiafya.