Muuguzi wa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya San Gerardo nchini Italia, Daniela Trezzi (34) amejiua baada ya kupata maambukizi ya COVID_19 na kuhofia kuwa atawaambukiza wengine

Mbali na hofu ya kueneza Virusi hivyo, imeelezwa kuwa Daniela pia alikuwa na msongo wa mawazo uliosababishwa na kazi kubwa wanayofanya watumishi wa afya katika kudhibiti CoronaVirus

Kabla ya kifo chake aliwaambia wafanyakazi wenzake kuwa ana wasiwasi amemuambukiza mtu mwingine Virusi hivyo uchunguzi zaidi wa kifo cha DanielaTrezzi unaendelea