Mvua ilianza kunyesha siku ya Jumapili saa tatu usiku na kuathiri kundi la wataliii 285 walikokuwa wanazuru mlima wa Gaohu mjini Yichun ambapo watu watatu wamefariki na wengine 23 hawajulikani walipo baada ya mvua huyo kunyesha na kusababisha mafuriko katika mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China.

Serikali ya nchi hiyo imewatuma waokoaji zaidi ya 530 katika eneo hilo kwa shughuli ya kuwaokoa majeruhi na kutoa misaada zaidi.