Mwana Fa afunguka sababu ya kuanzisha ‘Body Spray’ yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mjumbe wa kamati baraza la sanaa taifa (BASATA) Mwana Fa, ameamua kujiingiza kwenye biashara ya kuuza  perfume (Body Spray) aliyoipa jina la ‘FYN by FALSAFA’.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram msanii huyo ameeleza mengi ikiwa pia sababu iliyopelekea kuanzisha bidhaa hii ambayo ameungana na baadhi ya wasanii waliofanikiwa kuanzisha kitu chao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Alikiba ambaye alianzisha Tshirt za King Kiba pamoja na kofia lakini pia akaanzisha kinywaji chake kinachojulikana kama Mofaya, mwingine ni Diamond Platnumz ambaye ameanzisha vitu vingi sana ikiwemo Tv, Radio,lebo ya muziki,Karanga,Perfume na vingineo vingi, pia Mwana Fa ameungana na wasanii hawa na wengine kuwa katika rodha ya wasanii wanaomiliki bidhaa zao.

Alichokieleza Mwana Fa:- ” Since wameamua kunifurahisha kwa kumfukuza Mreno,na mi nimeona tujifurahishe tu wenyewe pia na sisi,tunukie tu vizuri..kwani kitu gani bwana 😀
Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays zetu hizi hapa @FYNbyFalsafa; blue ya kiume na pink ya kike… imagine bei ya jumla ni TZS 4,000 kwa moja, SHANGAA WEWE, na niamini zitafanya unukie vizuri SANA…😀
Kuanzia wiki ijayo mzigo utakuwa madukani. Yeyote anayetaka kufanya pre-order ama kuwa msambazaji wasiliana nasi kwa namba +255766170270 au email management@mwanafa.com; nawashukuru kabisa. 🙏🏽
| Smell FYN | Be FYN | #FYNbyFalsafa |”

Baadhi ya wasanii waliompongeza ni pamoja na Alikiba, Idris Sultani, Ay na baadhi ya wadau wengi wa burudani: