Mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu ‘MwanaFA’ ametangaza kuwa na maambukizi ya virusi hivyo jana ambapo amesema alirejea Jumanne kutoka Afrika Kusini na akawa hajisikii vizuri kiafya

Mwana FA amesema kwa sasa amejitenga na anaendela vizuri na hali ya joto aliyokuwa anaisikia awali sasa hivi haisikii tena na anaendelea vema huku akiwasihi Watanzania kujikinga zaidi

Aidha Mwana FA amewatoa hofu Watanzania na kuwataka wazingatie kanuni bora za afya kama zinavyoelekezwa na wataalam.

Hata hivyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amempongeza msanii huyo wa muziki wa Hip Hop Mwana FA kwa kumuona yeye kama ni jasiri na kwamba ataweza kupambana na kuushinda ugonjwa wa Corona.