Mwanamke ambaka mtoto wa miezi 9

Janet Auma ambaye ni dada wa kazi anatafutwa na Jeshi la Polisi Nchini Kenya kwa tuhuma za kumjeruhi sehemu za siri mtoto wa bosi wake mwenye umri wa miezi 9.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuingiza vidole sehemu za siri mtoto huyo na kumjeruhi vibaya, huku akisema kuwa mizimu ya babu yake ndiyo iliyosababisha kufanya kufanya kitendo hicho.

Mama wa mtoto, Benadeta Mukami amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa mtoto wake wa kiume, ambapo alimpigia simu akiwa kazini na kumwambia kuwa mtoto anatokwa na damu sehemu za siri, na kuagiza amtoe pempers.

“Walipomtoa nepi, mtoto wangu wa kiume alinipigia na kunitaka nirudi nyumbani haraka, kwani tatizo lilionekana kuwa ni kubwa, na tukamkimbiza hospitali”, amesema mama wa mtoto huyo, Bi. Bernadeta.

‘Walipomaliza kumfanyia vipimo, daktari aliniambia hawajakuta mbegu za kiume lakini sehemu za siri za mtoto zimeingiliwa na kuumizwa”, aliendelea kusimulia mama huyo.

Baada ya mahojiano na msichana huyo alimwambia mjomba wa mtoto kuwa alikuwa anasumbuliwa na mizimu ya babu yake, na alitumia vidole kumuingilia mtoto huyo mwenye miezi 9 mara kadhaa, na hata hivyo alikimbia kabla hajachukuliwa na polisi.