Mwanamume mmoja wilayani Apac nchini Uganda, aliyefahamika kwa jina la Moses Okot (46) amekatwa sehemu zake za nyeti na mke wake, Beatrice Acen (35) kwa madai kuwa mke huyo amekosa huduma ya unyumba kwa muda wa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo, Limeeleza kuwa tukio hilo limetokea Jumapili iliyopita ya Juni 30, 2019 ambapo mke wa mwanaume huyo, Alirudi nyumbani akiwa amelewa na kisha kumkata mme wake uume akiwa usingizini.

Mwanaume huyo alielezea tukio hilo kwa kusema “Nilirudi kutoka kuwinda majira ya saa 1 usiku, Mke wangu hakuwepo nyumbani. Binti yangu akanipa chakula na baada ya kula nikaenda kulala. Mke wangu aliporudi majira ya saa 4 usiku alifoka nimfungulie,”.

“Kwa wakati huo mimi nilikuwa tayari nimelala usingizi, Baadae kidogo nikahisi kama maumivu kwenye sehemu zangu za siri na damu ikinitoka, Huku yeye akiwa pembeni kitandani ameshika kisu  akiwa amelewa,”ameeleza Okot na kusimulia chanzo cha ugomvi na mkewe.

Mke wangu amekuwa mlevi wa kupindukia, Na tuna muda kidogo tupo kwenye mafarakano ya kifamilia hivyo niliamua tuishi bila kufanya mapenzi ili aweze kubadilika kwani amekua kila akilewa akihitaji tufanye mapenzi na mimi namkatalia,“ameeleza Okot.

Imeelezwa kuwa Okot na mkewe wameishi kwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10 na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.

Kwa upande mwingine, Menyekiti wa Kijiji cha Amin B, Anthony Ogwal ambacho wawili hao wamekuwa wakiishi, Amesema wanandoa hao wamekuwa wanagombana mara kwa mara na sababu kubwa ikiwa ni mwanamke kulalamikia unyumba.

Si mara ya kwanza Acen anamuumiza mumewe. Mwaka jana alimvunja mfupa wa bega wakati wanapigana na akakimbia. Shauri lilimalizika katika ofisi yangu na wakarudiana, Hili ni tukio la pili sasa linatokea.” Amesema  Ogwal. 

Baada ya tukio hilo, Okot alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Olelpek kufungua kesi dhidi ya mkewe na Jalada kupelekwa katika hospitali ya Apac anakoendelea na matibabu. Polisi wamesema shauri limefunguliwa na kupewa RB namba SD04/30/06/2019 na amepewa fomu ya polisi ya matibabu.