Chuo cha mafunzo Zanzibar kimemkamata bi Khadija Hashim Mussa mkaazi wa Tomondo kwa tuhuma za kuingiza ndani ya chuo hicho dawa za kulevya zinazosadikiwa kuwa ni kokein.

Mtuhumiwa huyo ameingiza dawa hizo kupitia nguo alizompelekea mumewe aliye katika mahabusu ya chuo hicho kilimani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kilimani kamishna wa chuo cha mafunzo zanzibar  Ali Abdalla Ali amewataka wananchi wa Zanzibar  wenye ndugu zao chuoni kwa  makosa tofauti kutotumia fursa ya kuwakagua kwa kuwapelekea vitu visivyo kubalika kisheria.

Amesema chuo cha mafunzo kipo makini katika kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Hata hivyo kamishna Ali amewataka wananchi kuendelea kuwatembelea ndugu zao waliopo katika vyuo vya mafunzo kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

Rauhiya Mussa Shaaban