Mwanamuziki Mkongwe na gwiji wa muziki katika miondoko ya Country, Mmarekani Kenny Rogers amefariki usiku wa kuamkia leo huko Sandy Springs, Georgia, Marekani

Familia yake imesema Rogers aliyekuwa Mwandishi wa Nyimbo, Muigizaji, Muimbaji na ‘Producer’ amefariki kwa amani (peacefully) akiwa chini ya Uangalizi wa Muuguzi huku akiwa amezungukwa na familia yake

Rogers, alitamba kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo The Gambler, Lady, Islands in the Stream na Lucille, huku akiwa ameuza rekodi zaidi ya Milioni na kushinda tuzo 3 za Grammy.