nairobi

Mwanasiasa wa upinzani ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Stephene Mukabana ambaye kiongozi wa vijana wa chama cham Orange Democratic Movement (ODM), aliuawa usiku wa jana wakati akienda kumsaidia mtu mmoja aliyekuwa akiporwa na kundi la watu sita kwa mujubu wa gazeti la Standard nchini humo.

Pia gazeti la Standard lilimnukuu gavana wa Nairobi Evans Kidero akisema kuwa kundi la wauaji limemfuata na kumuua mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 42.