Mwanza ya Rayvanny na Diamond yarudi kimya kimya

Baada ya Rayvanny kuiamriwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuifuta video ya wimbo wakeMwanza katika mtandao wa YouTube kwa madai kuwa haina maadili, leo Novemba 16, 2018, Rayvanny ameirudisha tena video hiyo YouTube kupitia Channel yake.

Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka Basata wala kwa Lebo ya WCB ambayo inammiliki msanii Rayvanny kuhusiana na video hiyo.

Video ya Mwanza mpaka wakati huu ni Trending namba Youtube huku ikiwa na watazamaji zaidi ya million 2.4 kwa muda wa siku tano.