Tumezoea kuona bidhaa nyingi zikibuniwa na watu kutoka mataifa ya nje nasisi kuishia kununua tu, lakini wapo vijana wabunifu wenye uwezo wa kutengeneza vitu vyenye thamani kubwa katika kisiwa chetu cha Zanzibar.

Silima Borafya Silima mkazi wa Kisonge Mjini Unguja ni Mjasiriamali anayetengeneza Sofa za kisasa, Meza na viti vyake pamoja na Dressing table kwa kutumia Pipa za mafuta.