“Nafsi yangu kama zilivyo nafsi zenu imegubikwa na huzuni kwa kuondokewa na Ndugu yetu, Kaka yetu, Mwenzetu Mkapa, katika hali kama hii muhimu ni kumuombea Mwenzetu kama ana makosa Mungu amuwie radhi, Mkapa alikuwa mtu mwema sana na mfanyakazi kwelikweli” -Mwinyi

“Mimi nimevaa viatu mara 2, nilipokwenda jandoni na ya pili nikiwa na miaka 13 nilichuma karafuu nikapata hela nikanunua viatu na nikataka visiishe badala ya kuvivaa nikavitunza, leo naona wote mmevaa viatu, ndio kazi ya viongozi ilifanywa na Mkapa na waliofuatia” -Mwinyi