Mwanamke mwenye umri wa miaka 104, kutoka nchini Italia ameweka rekodi mpya ya kupata maendeleo mazuri ya kiafya baada ya kupambana na ugonjwa unaosabbaishwa na Virusi vya Corona.

Mzee huyo aitwaye Ada Zanusso alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona, amepata ahueni wakati akipatiwa matibabu nyumbani kwake Biella Kaskazini mwa nchi ya Italia

Daktari ambaye alikuwa anampa matibabu mama huyo amesema kuwa, “Ameweza kuamka kutoka kitandani wala sio uongo na anaweza kutembea kwenda kwenye kiti chake, kuendelea kwake vizuri ni furaha kwetu na inatupa matumaini kwa wote wanaoumwa kwa wakati huu mgumu