Mahakama ya Wilaya Bukoba chini ya Hakimu mkazi Samweli Maweda imemuhukumu miaka 30 jela mzee wa miaka 70 kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 11 wa kata ya Maruku halmashauri ya wilaya Bukoba Mkoani Kagera.

Akiongea nje ya mahakama Wakili wa serikali mkoa wa Kagera Emmanuel Kahigi amesema kuwa tukio hilo lilitokea mwezi wa sita mwaka jana na kuongeza kuwa sambamba na mzee huyo aliyehukumiwa leo pia baba mzazi wa mtoto ameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika kosa hilo na kesi inaendelea.