Babu wa miaka 94 ameripotiwa kujinyonga hadi kufariki dunia jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema marehemu hajatambuliwa jina lake.

Muliro alisema kuwa marehemu alikutwa amejinyonga kwa kutumia mtandio uliofungwa juu ya mti wa mwembe pembezoni mwa nyumba yake.

Alisema chanzo cha kifo chake hakijulikani na polisi wanaendelea na uchunguzi.