Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kama ifuatavyo:-

1.Tarishi Daraja la III “Nafasi 1 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kufaulu.

2.Afisa Takwimu Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4.Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Stashahada katika fani ya Kutunza Ghala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

5.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 20 Machi,, 2019 wakati wa saa za kazi.