Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba Maji na Nishati Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI:

1.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Kutunza Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Afisa Usafiri Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafirishaji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3.Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

4.Afisa Uhusiano Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Shahada ya Kwanza ya Uhusiano wa Umma (Public Relation) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

5.Dereva Daraja la III “Nafasi 1 ” Unguja na “Nafasi 1 ” Pemba

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Form IV na kupata Mafunzo ya Udereva na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6.Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari 

7.Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Rasilimali Watu/Uongozi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2” Pemba 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

IDARA YA MIPANGO SERA NA UTAFITI:

1.Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Shahada ya Kwanza ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

IDARA YA NISHATI NA MADINI:
1.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Kutunza Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Geology Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Geology au inayohusiana na hiyo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

KAMISHENI YA ARDHI:

1.Mthamini wa Ardhi Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mthamini wa Ardhi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2.Field Assistance Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Mwenye elimu ya Sekondari na kupata cheti.

3.Afisa Mipango Miji Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango Miji na Vijijini kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4Dereva Daraja la III “Nafasi 1 ”

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Elimu ya Form IV na kupata Mafunzo ya Udereva na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

5.Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari 

6.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2” Pemba 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

WAKALA WA MAJENGO:

1.Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Shahada ya Kwanza ya Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2.Mhudumu /Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari 

3.Mpima Ardhi Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya “Geomatics” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

MAHKAMA YA ARDHI:
1.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 4”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 
ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 22 Machi, 2019 wakati wa saa za kazi.