Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kama ifuatavyo:-

OFISI YA FARAGHA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS UNGUJA:

1.Mpishi Daraja la III “Nafasi 1” – 
Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu mafunzo ya Upishi kwa ngazi ya Cheti au stashahada kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2.Afisa Takwimu Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Takwimu au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Fundi Bomba Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Cheti au stashahada katika fani ya Ufundi Bomba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

4.Fundi Umeme Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme (Electrical Engineering) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI:
1.Afisa Kumbukumbu Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2.Dereva Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva.
•Awe na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
•Mwenye Ufundi wa Magari atazingatiwa.

OFISI YA FARAGHA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS PEMBA:
1.Mwangalizi wa Majengo Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

TUME YA UKIMWI PEMBA:
1.Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2.Afisa Kumbukumbu Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

TUME YA UKIMWI UNGUJA:
1.Mhudumu Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari 

2.Dereva Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva.
•Awe na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
•Mwenye Ufundi wa Magari atazingatiwa.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 
ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g)Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 18 Aprili, 2019 wakati wa saa za kazi.