Nafasi za kazi Ofisi ya Mufti Zanzibar

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Mufti kama ifuatavyo:-

1.Afisa Fat-wa Daraja la II “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria au masomo ya Kiislamu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
•Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiarabu.

2.Dereva Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Sekondari na kupata cheti cha Udereva.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI, S. L. P 1587
ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 31 Agosti, 2018 wakati wa saa za kazi.