Nafasi za Kazi zaidi ya 160 Wizara ya Afya Zanzibar

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Afya Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Wauguzi Daraja la III “Nafasi 35” Unguja na “Nafasi 15” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uuguzi (nurse) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Wahudumu wa Afya (Ordalies) Daraja la III “Nafasi 15” Unguja na “Nafasi 10” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kufaulu

3. Fundi Sanifu Madawa Daraja la III “Nafasi 20” Unguja na “Nafasi 10” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ufundi Sanifu wa Madawa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Fundi Sanifu Maabara Daraja la III “Nafasi 4 ” Unguja na “Nafasi 3” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ufundi Sanifu Maabara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Afisa Tabibu Daraja la III “Nafasi 10” Unguja na “Nafasi 10” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Clinical Officer’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

6. Afisa Tabibu Meno Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 3” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Dental Therapist’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

7. Physiotherapist Daraja la III “Nafasi 3” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Physiotherapist’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

8. Afisa Afya Mazingira Daraja la II “Nafasi 6” Unguja na “Nafasi 4” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya katika fani ya Afisa Afya Mazingira (Environmental Health) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 3” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. Dereva Daraja la III “Nafasi 3” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na awe amepata Leseni ya Udereva.
• Awe amepata mafunzo ya Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

11. Muhandisi Ujenzi Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhandisi Ujenzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

12. Walinzi Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

13. Afisa Ushauri Nasaha Daraja la II “Nafasi 2” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ushauri Nasaha kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 28 Juni, 2018 wakati wa saa za kazi.