Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amezungumzia wimbo mpya wa Rayvanny na Diamond uitwao Tetema.

Katika mahojiano na Wasafi TV amesema kuwa ni wimbo mzuri na mara kadhaa ameusikiliza, huku
akimpongeza Diamond kwa kazi nzuri.

“Ngoma yake nimeisikiliza inaitwa Tetema, yes, nimesikiliza ni wimbo mzuri. Diamond anafanya
vizuri, ni muimbaji mzuri, wimbo wote ni mzuri,”
amesema.