Naibu Waziri alaani vikali wenyetabia ya kukata miti ovyo

Naibu waziri wizara ya kilimo, maliasili , ufugaji na uvuvi Zanzibar Dk Makame Ali Ussi  amesema kitendo cha baadhi ya wananchi kukata miti ovyo pasi na kufuata sharia ni kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mpenda maendeleo kwani athari zake ni kubwa ikiwamo kuchangia
mabadiliko ya tabia nchi hatimae kuiacha nchi ikiwa na  joto kubwa.

Alisema dunia inajitahidi kupigana na mabadiliko ya tabia nchi na Znazibar ikiwa ni sehemu ya dunia  nayo imo katika jitihada za kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi hayaathiri kupitiliza visiwa hivi.

Dk Makame alisema kuna baadhi ya wananchi bado wanamiliki misumeno ya moto na wanaitumia vibaya hivyo wanapaswa kufuhamu kuwa kukata miti ovyo ni kuharibu mazingira na misumeno wanayoitumia haikubaliki kisheria , hivyo atakaetiwa hatiani sharia itachukuliwa dhidi yake.

“hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu kukata miti ovyo  kwa chein saw, badala yake inatakiwa itumie kihalali , sasa tutasachi nyumba hadi nyumba kuitafuta misumeno hiyo maana taarifa zinaonyesha bado
ipo”
alisema Naibu huyo.

Katika kulitilia mkazo umuhimu wa kuyahifadhi mazingira Naibu Waziralisema “kuna mtalaamu wamazingira aliwahi kuandika kitabu akisema –
dunia ni kiumbe hai unapokata miti ni sawa na kumnyonyoa mtu kichwa”

alisema

Aidha ameipongeza taasisi ya Jumuiko la Kupambana na Mabadiliko yaTabia nchi Zanzibar kwakua imeonyesha nia ya dhati kuyahifahdi mazingira ya nchi ikiwamo kuendesha miradi mbalimbali sambamba na
kuwapatia elimu asasi za kimazingira na wananchi wa kawaida , alisema jambo hilo linapaswa kupongezwa.

Awali akimkaribisha Naibu waziri , Mkugenzi kutoka idara ya misitu na mali zisizohamishika Zanzibar Soud Mohd  Juma  alisema, mabadiliko ya tabia nchi yameshaanza kuathiri visiwa vya Unguja na Pemba hivyo jitihada za haraka zinatakikana kuiepusha nchi kutumbukia katika balaa hilo.

Alisema, kwa tathmini ya haraka haraka katika kisiwani Pemba mashamba 147 yameingiliwa na maji chumvu na hivi sasa yahafai kwa shuhuli za
kilimo, alisema hayo ni matokeo ya watu kukata miti ovyo pamoja na kutohifadhi mazingira.

“katika miaka 1990 Zanzibar kulikua na Paa Nundu 6,000 lakini hivi
sasa waliyobakia hawazidi 600, misitu inavamiwa na kukatwa hawawezi
kubakia, kuna hatari tukabakia watu tu tukaanza kulana wenyewe”

alisema Mkurugenzi huyo.

Sambamba na hayo Mkurugenzi aliipongeza taasisi ya ZACCA kwa kujitolea kupigia mbio uhifadhi wa mazingira Zanzibar huku akisema serikaliimeshaweka mikakati madhubuti hasa kwa kushirikiana na taasisi kama
hiyo.

Amina Yussuf Kashoro Mwenyekiti wa Jumuiya la Kupambana na Mabadiliko ya Tabia nchi Zanzibar alisema, taasisi yao imeundwa baada ya kukusanyika vijana ambao walihisi hakuna budi kujitolea kuhifadhi
mazingira ya nchi hii.

“ tumekua tukifanya shuhuli mbalimbali zinazohusiana na mabadiliko ya
tabia nchi na kikubwa Zaidi taasisi hii imeanzishwa kwa lengo la
kuiona Zanzibar inakua na muhimili mzuri wa kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi”
alisema Kashoro.

Akiwasilisha mada ya Mabadiliko ya Tabia nchi mbele ya asasi tofauti zilizohudhuria mkutano huo , Mratibu wa Mradi wa uimarishaji uwezo na usimamizi wa asasi za kiraia juu ya mabadiliko ya tabia nchi na uhifadhi waBAO ANUAI Habiba Juma Abdallah alisema Mabadiliko ya tabia nchi ni mabadiliko makubwa ya mfumo wa hali ya hewa ambayo hutokea na hudumu kwa muda mrefu (miongo kadhaa mpaka milenia) hayo hutokea katika viashiria ya hali ya hewa ikiwemo joto, mvuwa, muelekeo wa upepo na mganandamizo wa hewa.

Akielezea kuhusu athari za mabadiliko ya Tabia nchi alisema kuongezeka kwa joto, kutotabirika kwa vipindi vya mvua, Kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwemo  matukio yanayotokae na bila ya kujirudia
(vimbunga) ukame na mafuriko.

Abdallah alisema mbinu za kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ni Kupewa kipao mbele maswala ya mabadiliko ya tabianchi ili wananchi wawe na
elimu ya kutosha.

Washiriki wa mkutano huo kwa pamoja waliipongeza ZACCA kwa kujitoa kusaidia kuikinga nchi na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa taalama hasa kwa asasi za kiraia

Mmjoa miongoni mwa washikiriki  kutoka MYDO,  jumuiya inayohusika na maendeleo ya vijana aliyejitambulisha kwa jina la Ali Kombo Hassan
alisema, mkutano huyo umemfaidisha sana hasa kufahamu njia mbalimbali za kuzitumia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

tumepata kujua zaidi athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, kwa sababu kukontrol mabadiliko haya inakua ngumu kidogo, mana
yanatokea muda mrefu lakini athari zake tunaweza kuzizuzia, mfano tunaweza kuwahamashisha jamii kupanda miti ya mikoko pembezoni mwa bahari ili kuzuia maji yasije juu”
alisema Hassan.

Taasisi mbalimbali zilihudhuria mkutano huo na miongoni mwa hizo ni ZAZOSO, ZAYEDESA, Idara ya Mazingira, ANGOZA pamoja na wanafunzi kutoka skuli mbalimbali.