Rais Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden wamekabiliana kwa mara ya kwanza katika mdahalo uliorushwa kwa njia ya televisheni kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba.

Wakati wa mdahalo huo uliochukua dakika 90, wagombea hao walikabiliana kwa kila jambo walichokuwa wanazungumzia kuanzia uchumi hadi namna ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Wagomebea hao walikabiliana juu ya ni watu wangapi Marekani wenye magonjwa yanayowaweka katika hatari ambako kunaweza kusababisha baadhi yao wasiweze kupata huduma ya bima ya matibabu.

Bwana Biden alisema kulikuwa na watu milioni 100 ambao tayari wana maradhi mengine lakini rais Trump alisema kuwa idadi hiyo ni uwongo mtupu.

Trump agusia rekodi yake ya kufanikisha mambo

Ikiwa kuna ujumbe kampeni ya Trump inataka Wamarekani kuchukua kutoka kwa mjadala huu – kipande cha picha ya video ambacho kilitumwa kwenye akaunti ya rais hata wakati mdahalo ulikuwa ukiendelea – ni kwamba Joe Biden alikuwa na karibu nusu karne katika ofisi ya Umma kutatua shida zinazokabili nchi, na shida hizo bado zipo.

“Katika miezi 47, nimefanya zaidi ya vile umefanya kwa miaka 47,” Trump alimwambia makamu wa rais.

Jibu la Biden lilikuja baadaye kwenye mdahalo.

“Chini ya rais huyu, tumekuwa dhaifu, wagonjwa, masikini na tumegawanyika zaidi,” alisema.

Uchambuzi unaendelea