Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nay wa Mitego ameamua  kutoa ya moyoni kuhusu vuguvugu linaloendelea baina ya matamasha makubwa yanayotarajiwa kufanyika wikiendi hii nchini Tanzania.

 

Matamasha hayo ni Fiesta ambalo litafanykia  Dar Es Salaam, jengine ni Wasafi Festival litakalofanyika Mtwara na la mwisho ni lile litakalofanyika Kahama ambapo Alikiba ataenda kuperform na kundi lake la Kingsmusic,

Msanii huyo amefunguka na kusema :-

Mmh Nasubiri Kuona List Ikiendelea But Mmh. Awa Mbona Hawana Maajabu.?! Waimba Bure Wote Ninao Waona Apa😂😂 Hawapatagi Show Ata Za Bure Awa. Oyaa Nataka Kuona List Ya Wasanii Heavy Sio Awa Wasio Julikana Ata Makwao Kama Wanaimba🎤😂 Msiniangushe Wazeeeeeeeee.! …….
#Tar24. Wanangu Wa Dar Hakikisheni Mnaenda #Leader‘s Kwa Wingiii. Wanangu Wa Mtwara Hakikisheni Mnajaa Pale #Nangwanda. Na Machizi Wangu Wa #Kahama Inabidi Mkajae Pale #UwanjaWaTaifa. 
Mkifika Sehemu Zote Wapeni Salamu Zangu #HakunaMaishaMagumu“