Kwa mujibu wa Oxfam, Zaidi ya watu milioni 52 katika nchi 18 Barani Afrika wanakabiliwa na baa kubwa la njaa, sababu ikiwa hali mbaya ya hewa, umasikini na migogoro.

Baadhi ya maeneo yana ukame kwa kipindi cha miaka minne huku nchi nyingine, ukame umefuatiwa na mafuriko makubwa kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na mabadiliko ya vipindi vya hali ya hewa vya kawaida.

Related image

Hali hii ni mbaya kwa nchi kama Angola, Malawi, Msumbiji, Madagascar, Namibia na Zimbabwe.
Ukame umeathiri Mashariki na eneo la Pembe ya Afrika hasa Ethiopia, Kenya na Somalia, ikiharibu mazao na mifugo. Mazao ya nafaka katika baadhi ya maeneo yamepanda bei, gharama ambazo watu walio masikini wa vipato wanashindwa kumudu

Wakati huohuo, joto la juu katika Bahari ya Hindi imesababisha mvua kubwa nchini Kenya na Sudani Kusini, na kusabisha mafuriko makubwa ambapo Sudan Kusini ilitangaza hali dharura baada ya watu zaidi ya 900,000 kukumbwa na mafuriko