Waziri wa Elimu Tanzania Prof. Joyce Ndalichako amesema Mitihani ya Kidato cha 6 itaanza Juni 29, na kumalizika Julai 16, 2020, na mitihani hiyo itaenda sambamba na ile ya Ualimu na kulitaka Baraza la Mitihani kuhakikisha wanasambaza ratiba inayoonesha mitihani itakavyofanyika.

Ndalichako amesema Wanafunzi wa Kidato cha Sita watafungua Shule Juni 01, 2020 na wale wanaosoma Shule za bweni wametakiwa kuanza kuripoti Mei 30 watakuwa wakijisomea na kufanya maandalizi mpaka Juni 28, 2020.


Aidha, Waziri pia ameagiza Baraza la Mitihani (NECTA) kuhakikisha matokeo ya mitihani hiyo yanatoka kabla ya Agosti 31, 2020 ili wanafunzi hao waweze kujiunga na Vyuo Vikuu, kama ambayo Rais ameelekeza –
Jana, Rais Magufuli alitangaza Vyuo Vikuu vitafunguliwa Juni 01 mwaka huu, siku ambayo Wanafunzi wa Kidato cha Sita nao watarejea Shule. Hii ni baada ya hali ya CoronaVirus nchini kuendelea vizuri