Ndege ya kwanza ya shirika la ndege la Rwanda imeanza safari zake nchini Tanzania kwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na abiria kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Meneja Shirika la ndege la Rwanda nchini Tanzania Jimmy Mitali ameeleza faraja yao baada ya kuanza kwa safari hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kadico inayosimamia uwanja wa KIA Christina Mwakatobe ameelezea ujio wa kuanza safari za ndege ya Rwanda hapa nchini umekuwa ni muhimu sana pamoja na ndege nyingine kutoka nchi za ulaya kwani inaonyesha kuwa nchi ni salama haswa katika ugonjwa wa Covid-19.