Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema hajapata taarifa yeyote juu ya kuzuiliwa kwa mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, na amemtaka Mbunge huyo kuandika barua ofisi ya Spika juu ya madai yake.

Ndugai Amesema Bunge lina taratibu zake na mtu unapokuwa hujapata mshahara huendi kudai kwenye mitandao, hivyo Lissu aulizwe kwanza kama amezifuata hizo taratibu?

kiukweli sijasikia lolote lakini hayo madai ya mshahara alimwandikia Spika barua kwamba hakupata mshahara wake na akajibiwa ni kwanini hakupewa mshahara wake“.

Bunge linataratibu kwani hata wewe ukiwa hujapata mshahara huwa unadai kwenye mitandao, hebu muulize kwanza yeye amezifuata hizo taratibu?” ameongeza Ndugai.

Unajua nyinyi mnawafanya wabunge kama Mungu watu ila wabunge ni kama watumishi wengine wa umma kama wewe unavyokuwa hujapata mshaharana Mbunge anatakiwa afanye hivyohivyo.”

Mapema leo Machi 14, 2019, katika mitandao ya kijamii ameonekana Mbunge wa Singida Mashariki akilalamikia juu ya kuondolewa kwa mshahara wake.