Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde amesema bado hawajatangaza matokeo ya kidato cha nne na kuwataka Wananchi kuachana na taarifa feki zilizosambazwa katika mitandao.

“Bado hatujatangaza matokeo na muda ukifika tutawatangazia kama ilivyo kwa miaka mingine na wananchi mtapata taarifa naomba muachene na taarifa feki katika mitandao,” alisema Dk Msonde.