Nicki Minaj amepigana chini na management yake iliyokuwa ikimsimamia kwa muda mrefu, Blueprint/Maverick Management Company.

Sababu ya Nicki Minaj kuacha kufanya kazi na Management yake haijawekwa wazi zaidi ya kuwa wameachana kwa makubaliano ya pande zote mbili, Inaripotiwa kuwa Minaj alikuwa ameshaachana na uongozi wake wakati anafanya “Suprise performance” wikendi iliyopita kwenye tamasha la Coachella.

Hii imekuja baada ya utata mkubwa wa mauzo ya album ya mwisho ya Nicki Minaj “Queen” na pia ziara yake ya muziki kusogezwa mbele na kuhairishwa kwenye baadhi ya miji kwasababu ya uandaaji mmbovu.