Mwanamuziki wa BongoFleva Tanzania Tunda Man,  amesema gari la aina ‘Land rover Discover 4’ alilomnunulia Mke wake, pesa zake zinatokana na michezo ya kubashiri ‘Betting’.

Tunda Man ameeleza hayo kupitia E-Newz ya East Africa Television, ambapo gari hilo alimpa kama zawadi katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, mwishoni mwa mwezi Julai, 2019.

“Mke wangu alikuwa na ndinga kabla ya kumnunulia, gari linazaidi ya milioni 50 na mkwanja nilioshinda mimi ilikuwa ni Milioni 40, ile pesa ya kubet niliyoshinda niliongezea kama milioni 16 kununua gari na asilimia nyingi ile pesa ya kubet nilimpa mke wangu pia” amesema Tunda Man.

Aidha Tunda Man ameendelea kusema, kuna kipindi mke wake alikuwa hataki awe anacheza michezo hiyo, lakini yeye alikuwa anataka amuoneshe kama michezo hiyo ina faida, ndiyo maana alivyoshinda alimpatia zawadi ya gari.