NMB watoa vifaa vya michezo kwa timu za Baraza la Wawakilishi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid amewataka Viongozi wa Bank kuendelea na utaratibu wa kusaidia jamii hususan katika masuala ya Maendeleo kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati Akipoke vifaa vya Michezo Vilivyotolewa na uongozi wa benk ya NMB kwa timu ya mpira ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili kuwasaidia katika timu zao zilizoandaliwa barazani hapo.

Amesema Bank ya NMB imekuwa ikihudumia wananchi wa makundi mbali mbali ikiwemo wakulima na wana michezo hivyo ni vyema kuendelea kuthamini juhudi za wateja wao kwa kusaidia katika sekta mbalimbali.

Akizungumzia vifaa hivyo Spika Zubeir amesema licha ya vifaa hivyo kuwa ni sehemu ya kuendeleza Mashirikiano na Umoja walio nao lakini pia ni kutawezesha Wawakilishi kuwa na afya njena kupitia Michezo.

Pia alitumia fursa hiyo kuomba uongozi wa benk hiyo kuendeleza mashirikiano yaliopo kati yao ili kuona mabadiliko ya kiuchumi na kimichezo yandelea kupatikana kwa wateja wote na kusifu hatua za NMB katika kusaidia wateja wake.

Amesema licha ya vifaa hivyo kuwa ni sehemu ya kuendeleza Umoja wao lakini pia ni kuwawezesha Wawakilishi kuwa na afya njena kupitia Michezo.

Aliuomba uongozi wa benk hiyo kuendeleza mashirikiano yaliopo kati yao ili kuona mabadiliko ya kiuchumi na kimichezo yandelea kupatikana kwa wote.

Meneja Bank ya NMB tawi la Zanzibar,  Abdalla Duchi alisema wataendeleza mashirikiano hayo ili kuimarisha mashirikiano walionayo kwa muda mrefu katika kuwaletea maendeleo wananchi.

 “Sasa tunatimiza miaka Saba tangu kuwa na ushirikiano na wajumbe wa baraza ,hivyo leo hii kupitia msaada Wetu huu ni moja ya kuona ushirikiano huo unaendelea zaid”alisema.

Amesema NMB wanafarajika sana kuona uongozi wa baraza pamoja na serikali kwa ujumla kutokana na kuwaunga mkono katika jitihada zao mbali mbali ikiwamo kufungua akaunti katika benk yao.

Kwa upande wake Juma Kimori kutoka makao makuu ya NMB dar es sallam akitoa taarifa za NMB Makao makuu, alisema wataendelea kudumisha ushirikiay huo hasa katika Michezo,ambayo ni sehemu ya kuweka afya bora. 

Meneja msaidizi wa timu ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, Nassor Salum ameahidi kuvitumia vyema vifaa hivyo,ili lengo la utolewaji vifaa liweze kufikiwa.

Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa na  Uongozi wa benk ya NMB ni pamoja na Jez la Mpira wa miguu na Mpira wa mikono seti moja moja, soks,shingad, pamoja na bukta .