Leo Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein amezindua jengo jipya ‘terminal III’ katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, jengo ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria milioni 1.6 kwa mwaka.

Hizi hapa ni nukuu mbalimbali za Rais wa Zanzibar katika hotuba yake akizindua jengo hilo.

“jengo hilo litasaidia sana kuongeza abiria namizigo kwa sababu lina uwezo wa kuchukua abiria milioni 1.6 kwa mwaka ambalo litapunguzamsongamano wa abiria katika kituo cha Pili cha uwanja huo”.

“Naamini kwamba kiwanja chetu cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume na kile cha Pemba vitaweza kufikia ubora kama ule wa “Heathrow” kilioko London Uingereza, au “Changi” kilioko Singapore na vinginevyo ambavyo ambavyo vinatajika kuwa viwanja bora na
vyenye shughuli nyingi duniani”.

“hivi sasa uwanja huo wa ndege una uwezo wa kupokea ndege kubwa tatu ainaya “CODE E” kwa wakati mmoja ambapo pia, huduma zote ambazo zinastahiki kuwepi katikakiwanja cha ndege cha kimataifa cha kisasa tayari yapo”.