Nyangumi mmoja amekutwa na kilo 100 za uchafu tumboni mwake punde baada ya kufariki .

Baadhi ya uchafu waliokuta ni pamoja na nyavu za kuvulia samaki, kamba za kufungia mizigo, mifuko na vikombe vya plastiki.

Wataalam wa maswala ya viumbe hai Uskochi wamesema bado hawana uhakika kama uchafu huo umechangia kwa kiasi kikubwa kifo chake.

Lakini wanaharakati wa mazingira wamekemea uchafuzi wa mazingira kuwa sababu ya vifo vya viumbe hai.