Watoto wawili wa kike, mmoja wa miaka miwili na mwingine wa miezi 6  wamefariki  dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Agosti 7  katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni  kibatari kilichokuwa kikiwaka, kuangukia godoro na chandarua.

Taarifa zinaarifu kuwa  wakati moto huo unaanza, mama wa watoto hao  alikuwa  amekwenda kwa jirani kuomba chumvi.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi amesema amepokea taarifa hizo na akatoa  rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari.