Usiku wa kumakia Juni 14, 2019 Ofisi za Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoani lindi zimeungua moto na kusababisha vitu vilivyokuwamo ndani kuungua moto.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Proudencia Protus amesema Jeshi la polisi limeanza uchunguzi unafanywa ili kubaini chanzo cha moto huo.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini, Cecil Mwambe amesema mali zilizochomwa ni pamoja na pikipiki mpya iliyokuwa ipelekwe wilayani Liwale kwa ajili ya shughuli za chama, kompyuta na nyaraka mbalimbali na kwamba taarifa zimeshatolewa polisi.

“Ni taarifa za kweli ofisi iliyopo Lindi mjini imechomwa moto usiku wa kuamkia leo muda wa saa nane usiku, ndani kulikuwa na pikipiki mpya ambayo ilikuwa ipelekwe Liwale kwa ajili ya zoezi la Chadema ni msingi, kompyuta ya chama na nyaraka mbalimbali. Taarifa imeshafikishwa polisi, hii ni baada ya zoezi la Chadema ni msingi kupamba moto,” amesema Mwambe.

Mmoja wanachama wa chama wa chama hicho, Juma Mwinga amesema ilikuwa majira ya saa nane usiku wakati tukio hilo linatokea baada ya jirani kusikia harufu ya moshi.

chanzo mwananchi