Dkt. Charles Mahera ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, amesema watu wenye mahitaji maalum watapewa kipaumbele kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28

Watu hao ni kama Walemavu, Wajawazito, Wanaonyenyesha, waliokwenda na wazee au wagonjwa hivyo watapiga kura mapema na kuondoka

Watu wasiojua kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini ili kuwasaidia. Pia, Wasiokuwa na uwezo wakuona watawekewa Maandishi ya Nukta Nundu au wanaweza kwenda na wanaowaamini kuwasaidia.

Aidha, wenye ulemavu wowote ule watawezeshwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo. Maelezo hayo yote yameshatolewa kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura