Okwi amchafua roho kocha wake

Katika hali isiyotarajiwa, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, Jumamosi iliyopita alimtibua kocha wake, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji katika mchezo wao dhidi ya Nkana FC.

Okwi, raia wa Uganda, alimtibua Mbelgiji huyo wakati alipotolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Shiza Kichuya. Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Nkana jijini hapa, ulimalizika kwa Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1.

Tukio hilo lilishuhudiwa ambapo Okwi alionekana kutokubali kutolewa mapema. Baada ya kutolewa, hakusalimiana na mtu yeyote mpaka anaenda kukaa kwenye benchi na hata alipopewa bips avae kwa zaidi ya mara mbili alikataa. 

 “Okwi hakuwa vizuri, niliamua kumtoa ili aingie mtu ambaye angeweza kuisaidia timu”Aussems alisem.

Ikumbukwe kuwa, baada ya mchezo huo wa juzi, timu hizo zinatarajiwa kurudiana wikiendi ijayo jijini Dar na mshindi wa jumla atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo na atakayetolewa anaenda kucheza ‘play off’ katika Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi, hivyo lazima ufanye vile kwa kumtoa mtu ambaye anaonekana hayupo mchezoni, lakini hilo alilofanya wala halinisumbui.”