Wamiliki  wa mahotel  kijiji cha Nungwi wamewataka wazazi na walezi  wanaoishi karibu na mahoteli kuwazuia watoto  na kuwakataza tabia ya kuomba omba watalii kwani hatua hiyo itaweza kuwasababishia kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. 

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa baadhi ya wamiliki wa mahoteli hao ambao wamekataa kutajwa majina yao wamesema tabia ya kuomba omb pia ni chanzo cha udhalilishaji kwa watoto kwani wapo baadhi ya wageni hawatoi pesa zao bure. 

Wamesema wazazi wanajukumu kubwa la kuwadhibiti watoto wao kwa kufatilia mienendo ya watoto ili kuwanusuru na vitendo vitavyo wafikisha kwenye majanga hatarishi. 

Wamesema mbali na udhalilishaji lakini pia tabia ya kuomba omba wageni wanaofika kwa ajili ya kufanya utalii visiwani Zanzibar  ni kuitia doa nchi na kuonekana Zanzibar  ni nchi  yenye njaa na umaskini mkubwa kwani watu wake wanaishi kwa kutegemea kuomba ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku. 

Wamesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imekuwa ikipiga kelele ongezeko la ombaomba maeneo ya mjini kwani wanachafua mandhari ya mji lakini hivi sasa ombaomba hao wamehamia  sehemu za mahotel  wakiwemo na watoto. 

” Endapo wazazi wahatolifatilia jambo hili watapelekea watoto wao kuwa katika wakati mgumu kwani kwa maisha ya sasa hakuna anaeweza kutoa msaada bila ya malengo”  walisema wamiliki wa mahoteli. 

Wamesema wageni wamekuwa wakisumbuliwa sana na watoto pamoja na ombaomba wanapokuwa kwenye fukwe kwa ajili ya kupumzika  hii inatoka na kutokuwepo udhibiti wa uhakika kwenye sehemu za fukwe kwa watu wasokazi maalum. 

“Watoto wanasumbua au kwavile shule zimefungwa hawana kazi za kufanya huko majumbani mbona wimbi kubwa la watoto wanaoomba wazungu jaman wazazi wadhibitini watoto wenu wanapotea”walisema kwa masikitiko makubwa wamiliki wa mahotel. 

Aidha wamesema  kutokana na hali hiyo hatua mbalimbali wanazichukua ikiwemo kuwafukuza watoto pindi wanapowaona wanazurura bila ya kazi maaalum ili kuondo vurugu ufukweni. 

Amina Omar