Wanafunzi walioteuliwa wanatakiwa kufika katika ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar zilizopo katika jengo la majestic cinema vuga kwa waliopo unguja na jengo la wizara ya elimu na mafunzo ya amali chake chake kwa waliopo pemba kuanzia tarehe 19/11/2018.

Inasisitizwa kila mwanafunzi aliyeteuliwa anapaswa kujaza mkataba maalum wa mkopo unaotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar kabla ya kuanza kupatiwa mkopo huo. Zoezi la utoaji mikataba kwa wanafunzi wapya litaendelea hadi tarehe 31/12/2018.

Wanafunzi walioteuliwa wanatakiwa kuchukua kitambulisho cha mzanzibari na “bank pay in slip” kuthibitisha kufanya malipo ya tzs 35,000 katika akauni na. 021108001357 ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar iliyopo katika benki ya watu wa zanzibar (pbz) wakati wa kuchukua mikataba.

INDHARI

Wanafunzi waliopata mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ya serikali ya muungano (heslb), majina yao yataondolewa katika uteuzi wa wanafunzi watakaopatiwa mikopo inayotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayepata mikopo kutoka bodi zote mbili kama sheria inavyoelekeza.

BONYEZA LIKI CHINI KUTAZAMA ORODHA YA MAJINA

WANAFUNZI WALIO TEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA

WANAFUNZI WALIO TEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA PILI

WANAFUNZI WALIO TEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA PhD