Kiasi cha Dola milioni 190 katika thamani ya soko baada ya mama mmoja mjamzito kukuta panya aliyekufa kwenye supu kwenye moja ya mikahawa ilioko nchini China.

Hisa za migahawa hiyo ya Hotpot imeporomoka vibaya, baada ya picha za panya huyo aliyekufa akitolewa kwenye bakuli la supu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mgahawa wake katika Jimbo la Shandong, umefungwa kwa muda.

Mkahawa huo ulimpa mama huyo Dola za Kimarekani 729 kama fidia kufuatia tukio hilo, lakini alizikataa.

Mwanamke huyo mjamzito ambaye alikwenda katika mkahawa huo pamoja na familia yake mnamo Septemba 6 alimuona panya aliyekufa wakati tayari akiwa amekula vipande kadhaa vya nyama kwenye supu.

Taarifa zaidi zinasema mmoja wa wafanyakazi wa mkahawa huo alimshauri mume wa mama mjamzito atoe mimba kama ana wasiwasi kuhusu afya ya kichanga chake na kuahidi kumpa fedha kwa ajili ya kuitoa mimba yake.