Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems yupo mbioni kuongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo msimu ujao baada ya bodi ya klabu hiyo kukaa na kuamua juu ya hatma yake.

Aussems ambaye alisaini mkataba wa muda mfupi ndani ya Simba, anatarajia kuingia katika mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuongeza mkataba mwingine mara baada ya huu wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe alisema lengo la klabu hiyo ni kuona wanafanikiwa kufika mbali zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hivyo wameona ni vyema kubaki na Aussems ili kufanya vyema.

“Suala la kocha Aussems la kuongeza mkataba lipo juu, bodi ambao ndiyo wanaoamua, kocha ataongeza mkataba wake mwingine kwa ajili ya kutumikia Simba ila kwa sasa mtazamo upo kwenye mechi zetu za ligi kuu kwanza.

“Levo ambayo Simba tumeifikia ni ya juu zaidi, tunahitaji kuendelea pale tulipofikia msimu huu katika mechi za klabu bingwa ili tuweze kufika mbali kwa kuendelea na kocha huyo.

“Pia kutafanyika tathimini ya mechi zake zote za ligi na za kimataifa kwa ajili ya kufanya maamuzi hayo,” alisema Kashembe.
Aussems