Paul Clement amkana mlezi wake

Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha mara nyingi amekuwa akionekana akiandika katika baadhi ya post zake kuwa yeye ndio mlezi wa wasanii wote wanaoimba injili nchini Tanzania na hata kuna baadhi ya mambo amekuwa akitaka kuyabeba majukumu akiwa kama mlezi wa nyimbo za injili.

Swali linakuja je , wasanii wanajua kuwa yeye ndio mlezi wao wa nyimbo za injili, jibu tunalipata kwa wasanii wenyewe kuhusu kiongozi wao huyo.

Mwanahabari Hassan Ngoma alipata fursa ya kuuliza swali hilo kwa msanii Paul Clement alipokuwa katika mahojiano asubuhi ndani ya 360 ya clouds media, na mwanainjili huyo alikata na kusema kuwa kwa upande wake yeye kiongozi wake sio Emmanuel Mbasha bali ni mchungaji wake.

Mmmh hapana , mimi mlezi wangu wa injili ni mchungaji wangu”
Paul anasema