Mradi  wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (PAZA) ulioundaliwa na TAMWA kwa kushirikiana na WAHAMAZA na NGENARECO pamoja na Asasi za kiraia  waibua maendeleo ya kimaisha kwa Wananchi wa Kaskazini Unguja.

Akizungumza na  Zanzibar24 blog Katibu wa Jumuia ya vijana kupambana na udhalilishaji Ali Makame Zuberi huko Gamba Wilayani Mkoa wa Kaskazini Unguja amesema katika mradi huo wamepata mafanikio makubwa ambayo kwakiasi fulani ipelekea jamii kuhamasika kwa njia tofauti za kimaisha.

Amesema  wamefanikiwa kufanya ziara mbali mbali kwa ajili ya kusambaza elimu ikiwemo elimu ya  udhalilishaji, kutoa mafunzo ya ujasiri amali kama vile kilimo, ufundi  charahani pamoja na ufumaji wa vitu tofauti kama mikoba, vipochi n.k

Wakati huo huo miongoni mwa Mjumbe wa Jumuia hiyo Sichana Othman Suleiman ameeleza kuwa Mradi wa uwajibikaji Zanzbar umewafumbua macho kwa kubuni miradi tofauti ya kujiwezesha kimaisha napia kuwajengea uwezo wa kupata fursa ya kuzitangaza biashara zao katika matamasha mbalimbali nchini.

Amesema katika Mkoa  wa Kaskazini Unguja hapo mwanzo hakukua na uelewa wa suala la udhalilishaji lakini baada ya kuwepo kwa mradi huo wamefanikwa kupata elimu na hatimae kuifahamisha jamii pindipo linapotokea tatizo hilo njia gani wapitie.Tumefanikiwa kumuhamasisha Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B kuhusu ndoa za umri mdogo nakwakweli tulifanikiwa maana kuna mwanafunzi aliolewa hatimae Mkuu huyo akaenda akaihairisha ndoa na kutoa maamuzi ya kutolewa talaka”amesema mjumbe huyo.

Ameeleza kuwa mbali na hayo pia wamefanikiwa kuwahamasisha wanafunzi watoro kurejea mashuleni ili kuendelea kupata elimu.”Kwakila mwanafunzi mtoro tumefanikiwa kumfuata na kumfahamisha hatimae kutuelewa na ifikapo januari wanafunzi wote watoro wataanza skuli rasmi”

Hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto wanazozipata katika mradi huo ni miongoni mwa ugumu wa kutofahamika  kwa wazee , napia uhaba wa vitendea kazi  katika shuhuli zao.

Akitoa ushauri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa Serikali itafute  mbinu tofauti za kuwatafutia wananchi kupata masoko ili kukuza biashara zao.